(ABNA24.com) Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, chimbuko la mizozo na migogoro katika eneo la Mashariki ya Kati ni hatua ya Israel ya kuvamia na kukalia kwa mabavu ardhi za Kiarabu ikiwemo miinuko ya Golan ya Syria.
Bashar al-Jaafari amesema hayo katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichoitishwa kwa ajili ya kujadili changamoto za amani na usalama katika Mashariki ya Kati na kueleza kwamba, eneo hili limekuwa likishuhudia matukio hatari na ya kutisha kutokana na siasa zisizo za kimaadili za madola ya kikoloni.
Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa amelaani vikali njama zilizoratibiwa za kupandikiza migogoro katika eneo la Mashariki ya Kati ambazo lengo lake ni kuzuia kuhitimishwa uvamizi na ukaliaji mabavu ardhi za mataifa mengine unaofanywa na utawala haramu wa Israel.
Kadhalika Bash al-Jaafari amevitaka vikosi vamizi vya Uturuki na Marekani kuondoka katika ardhi ya Syria.
Nchi za Marekani na Uturuki zimetuma wanajeshi wake nchini Syria kwa kisingizio eti cha kupambana na makundi ya kigaidi, hatua ambayo imefanyika bila ya ridhaa wala idhini ya serikali ya Rais Bashar al-Assad.
Serikali ya Syria hadi sasa imelaani mara kadhaa hatua hiyo ya serikali ya Uturuki na Marekani na kuzitaka Washington na Ankara kutoa wanajeshi wao katika ardhi ya nchi hiyo ya Kiarabu.
/129
21 Agosti 2019 - 08:23
Msimbo wa Habari: 970261
Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, chimbuko la mizozo na migogoro katika eneo la Mashariki ya Kati ni hatua ya Israel ya kuvamia na kukalia kwa mabavu ardhi za Kiarabu ikiwemo miinuko ya Golan ya Syria.